FAHAMU BAADHI YA MAGONJWA UNAYOWEZA KUJITIBU MWENYEWE KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA: ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa...
FAHAMU BAADHI YA MAGONJWA
UNAYOWEZA KUJITIBU MWENYEWE
KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA:
ZIKIWA zimesheheni protini na madini
kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia,
manganizi na zinki, mbegu za maboga
zinakuwa mbegu bora na muhimu
kutafuna kila wakati kama wewe ni
mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika
pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga
zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa
kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya
10:
01 UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha
madini aina ya maginizia (magnesium)
ambayo huboresha utendaji kazi wa
viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji
wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji
wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya
damu kupitisha damu kwa urahisi na
hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa
laini.
02 KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha
madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana
faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha
kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na
uundaji wa chembechembe hai za mwili,
kuboresha usingizi, kuboresha ladha
mdomoni na harufu, huboresha afya ya
macho na ngozi, hurekebisha sukari na
huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una
uhusiano mkubwa sana na matatizo ya
kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi
mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo
darasani kimasomo na matatizo mengine
mengi ya kimwili na kiakili.
03 MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu
sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na
mbegu za maboga ni miongoni mwa
mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina
hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga
utakuwezesha kupata kirutubisho hiki
muhimu katika mwili wako na kukupa
faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.
04 KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za
maboga zimetumika kuimarisha afya ya
wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi
sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni
muhimu sana kwa afya ya kibofu cha
mkojo. Mbegu za maboga pamoja na
mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa
kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo
ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya
kibofu.
05 KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu ambao hula
mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za
maboga wamegundulika kuwa na hatari
ndogo sana ya kupatwa na saratani za
tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
soma na hii: TIBA YA MAGONJWA
MBALIMBALI KWA KUTUMIA ASALI
06 UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama
mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji
wa mbegu za maboga, husaidia
kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini
na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na
ugonjwa wa kisukari.
07 MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu wazima
ambao wamefikia ukomo wa hedhi,
hupatwa na matatizo mbalimbali
yanayosababishwa na hali hiyo. Hata
hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za
maboga zina uwezo wa kurekebisha hali
hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya
yatokanayo na ukomo wa hedhi.
08 AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi
cha mafuta mazuri, kamba lishe na
virutubisho vinavyoimarisha kinga ya
mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa
bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza
kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya
kiafya katika moyo na ini.
09DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa
na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za
usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa
chache kabla ya kupanda kitandani, hasa
ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia
kupata usingizi mzuri na tulivu.
10 DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za
maboga zina mafuta yenye uwezo wa
kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe
(inflamatory diseases) sawa na dawa aina
ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi
hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo
dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za
mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo
zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia
unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri
ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi.
Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha
unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15,
unaweza pia kuongeza chumvi kidogo
kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa
hazina mafuta mengi kama zile kavu.....!
mwendelezo wa hii mada utafuata,
Endelea kutembelea kila mara kurasa
wetu, kufahamu huduma zetu zaidi.
Tupo; Chunbageni--Tanga mjini.
Pia tunatibu kiuhakika kwa kutumia Pia tunatibu kiuhakika kwa kutumia dawa
za miti shamba, haya ni baadhi tu;
# Ugonjwa wa Bawasiri ( kutokwa na
kinyama sehemu ya haja kubwa.
# Wahanga au waathirika na madhara ya
kujichua ( punyeto)
# Ukosefu / ama upungufu wa nguvu za
kiume.
# Uume uliosinyaa na kuwa mfupi.
# Korodani moja au zote kuvimba au
kuzama ndani.
# Matatizo mbali mbali ya wanawake
# Wanao wahi kufika kileleni haraka zaidi.
# Wasiohisi hamu ya tendo la ndoa,
COMMENTS